Thursday, February 21

ZANZIBAR: ZACADIA YAKABIDHI WHEELCHAIRS IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU!

0
AIMU Mkurugenzi Idara ya Diaspora Zanzibar Ndg. Hassan Khatib Hassan akimkabidhi msaada wa wheelchair Mkurugenzi wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Abdalla Rashid, vilivyotolewa na Wazanzibari wanaoishi Nchini Canada wa Jumuiya ya Diaspora ya ZACADIA. Kushoto ni Menaja wa Diaspora ya ZACADIA, Bi. Firdaus Rashid Rabia. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Idara hiyo Migombani, Zanzibar, tarehe 5 November, 2018.

MKURUGENZI wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Rashid Abdallah, akimkabidhi Wheelchair Ndg. Abubakar Abdulatif mlezi wa Mtoto mwenye Ulemavu Saleh Mustafa Mussa, baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Zanzibar Ndg. Hassan Khatib Hassan, katika viwanja vya Idara hiyo Migombani Zanzibar. Wheelchair hizo zimetolewa na Wazanzibar wanaoishi Nchini Canada, wa Jumuiya ya ZACADIA.

MKURUGENZI wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Rashid Abdallah, akimuendesha Mtoto mwenye Ulemavu Saleh Mustafa Mussa, baada ya kumkabidhi Wheelchair zilizotolewa na Diaspora ya Wazanzibari wanaoishi Nchini Canada wa Jumuiya ya ZACADIA.Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Idara hiyo Migombani Zanzibar tarehe 5 November, 2018.

(Picha na Ikulu)Share.

About Author

Leave A Reply