Sunday, August 18

WAZEE WA SHINYANGA NI HATARI!

0


BABU WA MIAKA 90 MBARONI KWA KUBAKA WANAFUNZI WATANO SHINYANGA

Babu aliyejulikana kwa jina la Kachuka Malongo (90) anashikiliwa na polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma ya kubaka wanafunzi watano wenye umri kati ya miaka 8 hadi 12 wa shule ya msingi Tinde A na B kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mapenzi ambapo mtuhumiwa aliwabaka watoto hao kwa nyakati tofauti akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa. 

Amesema tukio hilo la wanafunzi hao kubakwa limebainika Machi 21,2018 majira ya saa 2 na nusu asubuhi 

Kamanda Haule amesema wanaendelea kufanya mahojiano na mtuhumiwa na watamfikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Na Kadama Malunde- Malunde1 blog Read More

Share.

About Author

Comments are closed.