Saturday, August 24

Wazazi wa Azory Gwanda watoa ombi kwa Rais Magufuli!

0


Wazazi na ndugu wa mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Azory Gwanda aliyetekwa na watu wasiojulikana wamemuomba Rais John Magufuli kuagiza vyombo vya Dola kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kama yupo hai au amekufa.

Kwa mujibu wa mkewe, Anna Pinoni (35), siku hiyo asubuhi watu wanne wakiwa katika gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe, walifika katikati ya mji wa Kibiti, sehemu ambayo Azory hupatikana mara kwa mara, na kumchukua.
Watu hao walimpeleka hadi shambani ambako mkewe alikuwa akilima na akamuaga kuwa anaenda kazini, lakini hajarudi hadi leo.

Azory ambaye kituo chake cha kazi kilikuwa mkoani Pwani alichukuliwa na watu hao Novemba 21, 2017.

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply