Friday, July 19

Shirika la Direct Aid laendelea kusaidia Zanzibar kwa kuchimba visima vya maji 94!

0


Jumla ya Visima 94 vimechimbwa na shirika la la Direct Aid kwenye mpango kazi wa kusaidia jamii mwaka 2018 ili kupunguza tatizo la Maji ndani ya maeneo mbali mbali katika mji wa Zanzibar.

Akizugumza kwenye ufunguzi wa mwisho wa miradi ya Visima vya Maji mkuregenzi wa Shirika hilo Aiman kamal Din alisema miradi hiyo ya Maji imekuja kwa ajili ya kuisadia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Kushughulika na tatizo la maji linalowakabili wananjamii ndani ya Zanzibar.

Alisema mwaka 2018 miradi hiyo ya maji imeweza kusaidia sana maendeleo ya vijiji na mitaa unguja na Pemba kutatua kero ndogo ndogo hata kupunguza umbali wa kuyafata maji kwa waakazi wa shehia mbali mbali.Hata hivyo Aiman  Kamal Din alisema Shirika la Direct Aid lipo tayari kushirikiana na serikali kupitia wananchi wa Zanzibar pale ambapo panahitajika msaada wa kusaidia jamii ikiwemo miradi mbali mbali ya maendeleo kama vile Uvuvi,maji,bishara,ujenzi wa madrasa,misikiti,matibabu ya Afya vijjini, mikusanyiko ya futari, sadaka mbali mbali ndani ya jamii ya Zanzibar.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Sleman Ussi Pondeza moja ya majimbo yaliyofaidika moja kwa moja na miradi ya maji ndani ya Jimbo lake alipongeza shirika la Direct Aid kwa bidii yake kubwa ya kusaidia visima hivyo ambavyo wao kazi yao ni kuvutia umeme na kuvitunza ili kuweza kuusadia watu wa jimbo lake

Waziri wa kilimo Bishara na Uvuvi pia ni mwakilishi wa Jimbo la Amani Rashidi Ali Juma amelipongeza shirika hilo kwa moyo wake mkubwa baada ya kuchimba visima kwenye jimbo lake la Amani na Shehia mbali mbali za Unguja na Pemba kwa kuwa wanasaidia kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo.

Aidha amewataka wanachi wate waliosaidiwa na Shirika hilo kuhakikisha wanatumia fursa hiyo ndani ya Shehia zao kutunza mindombinu mikubwa hiyo ya Maji na miradi mengine mikubwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Mustafa Kitwana yeye hakuwa nyuma kulipongeza shirika hilo kwa kuleta huduma ya Maji kwenye kijiji Cha Muungoni wilaya ya Kusini Unguja kwa kuchimba visima kimoja kikubwa kikiwa na minara minne.

Visima hivyo vimechimbwa na kwenye Shehia mbali mbali za Unguja ikiwemo visima Vikubwa vilivyochimbwa eneo la Mwanakwerekwe, Magomeni,Magogoni, Amani na shehia nyengine .

Miradi hiyo ya Maji inaweza kuwafikia watu zaidi ya laki moja kwa kila eneo ili kuweza kutatua kero ndani ya jamii.

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply