Friday, May 24

Serikali yazungumza tena kuhusu Bandari ya Bagamoyo!

0


Serikali Imesema inaendelea na majadiliano kuhusu kuendelea na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani ili kuona kama inaweza kuwa na tija kiuchumi kwa upande wa Tanzania.

Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na East Africa Radio amesema si kweli kwamba serikali imeamua kuachana moja kwa moja na mradi huo.
“Serikali haijasema kuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari, tunaendelea na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, nchi yetu imejaliwa ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari kwa hiyo tuna uwezo wa kujenga Bandari nyingi tu” ameeleza.

“Hii ya Bagamoyo si kweli kuwa imeachwa kuna mambo ya msingi tunayajadili na tusipofikia maamuzi tutaachana nayo” amesisitiza Dkt Abbasi.

Kuhusu suala la uwekezaji wa vitu badala ya watu amesema, Serikali haitaacha kuwekeza kwenye vitu kwa sababu vitu husaidia maendeleo ya watu, mfano Afya, Elimu na Miundombinu mingine.

Share.

About Author

Leave A Reply