Thursday, February 21

Halima Mdee: Tunahitaji jamii ya watu huru wanaoishi bila hofu ya kutekwa!

0


Mbunge wa Kawe ambaye pia ni Waziri kivuli wa Fedha na Mipango , Halima Mdee alisimama Bungeni  kuwasilisha maoni ya mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambapo leo amelieleza Bunge kuhusu athari zinazoweza kujitokeza nchini kufuatia matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea kujitokeza mara kwa mara.

Halima katika mapendekezo yake pia amesema kuwa tunahitaji  kuwa na Bunge lenye kuikosoa Serikali na kuiwajibisha serikali.

“Baadhi ya wafadhili wameanza kukataa kutoa fedha kutokana na mwenendo wa siasa za nchi yetu usioridhisha, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni pamoja na watanzania wote tunalaani na tunapinga vitendo viovu vya ukandamizaji, utekaji na mauaji,” –Halima Mdee.


“Tunahitaji jamii ya watu huru  wanaoishi bila hofu ya kutekwa, kutengwa na wapendwa wao kuuawa au vitisho vya aina yoyote ile, tunahitaji kuwa na mahakama zilizo huru zinazotoa maamuzi yanayozingatia sheria na haki bila mashinikizo ya mtu yeyote, tunahitaji kuwa na tume huru ya uchaguzi inayofanya kazi kwa uhuru bila shinikizo la mtu au kikundi cha watu,” alisema Mdee.

“Tunahitaji kuwa na Bunge lenye kuikosoa Serikali na kuiwajibisha serikali. Tunahitaji Jeshi la Polisi linalozingatia sheria, usawa na haki za Binadam, Tunahitaji jeshi la wananchi lisiloegemea upande wowote na linalowajibika kwa wananhi wote wa Tanzania,” aliongeza.

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply