Sunday, August 18

MWAKIBINGA AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM, ATOA VIFAA VYA MAABARA SHULE YA UWKWAMANI

0


Balozi  wa vijana usalama barabarani James Mwakibinga akikabidhi  vifaa vya maabara kwa Afisa elimu wa kata ya Kawe Casmir Mavula na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kawe Ukwamani Safina Egha  alipotembelea shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BALOZI  wa vijana usalama barabarani James Mwakibinga ametoa vifaa vya maabara kwa shule ya Sekondari Kawe Ukwamani ikiwa ni katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhusu elimu bure.

Mwakibinga aliweza kutoa vifaa hivyo mbele ya wanafunzi na kuwataka kutilia mkazo katika masomo yao kwani hawawezi kufikia malengo yao kama watashindwa kusoma kwa bidii ikiwa kwa sasa serikali kupitia kwa Rais Dkt Magufuli ametoa tamko elimu bure kwa wote.
Balozi  wa vijana usalama barabarani James Mwakibinga akipata maelezo ndani ya maabara.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara na mifuko 20 ya saruji, Mwakibinga amesema kuwa ameamua kuunga mkono juhudi za Rais katika kuhakikisha  elimu bure kwa wote ikiwamo kusaidia kwenye vifaa mbalimbali vya mashuleni.

Mwakibinga amesema kuwa, wazo hili la kuwapatia shule ya Ukwamani vifaa vya maabara ili kuweza kuleta chachu ya wanafunzi kwenye masomo ya Sayansi kwani katika kufikia uchumi wa kati wa viwanda haina budi wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya sayansi.

Katika msafara huo wa utoaji vifaa vya mabaara Mwakibinga aliambatana na mwanafunzi bora wa kidato cha nne kutoka Kawe Ukwamani Faraji ambaye naye aliweza kushirikiana nae katika kuunga mkono jitihada za kusaidia vifaa kwa shule hiyo ambapo yeye alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne na kufanikiwa kupata ufaulu wa alama ya division 1.

Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kawe Ukwamani Safina Egha alimshukuru Mwakibinga kwa hatua kubwa aliyoifanya ya kuleta vifaa vya maabara kwa watoto hao ambapo amempongeza Rais Dkt Magufuli  kwa kuleta elimu bure na kuwasisitiza wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kuwa na maisha mazuri baadae.

Safina amesema kuwa ana imani wanafunzi hao wataleta tija katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu kutokana na jitihada wanazozionyesha katika masomo yao ikiwamo pia kupata vifaa vitakavyozidi kuwarahisisha kwenye matumizi ya maabara.

 Balozi  wa vijana usalama barabarani James Mwakibinga akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kawe Ukwamani  alipotembelea na kutoa vifaa vya maabara akiunga mkono juhudi za Rais Dkt Jaliohn Pombe Magufuli za elimu bure.

Balozi  wa vijana usalama barabarani James Mwakibinga akitembelea maktaba ya shule ya Kawe Ukwamani  alipotembelea na kutoa vifaa vya maabara akiunga mkono juhudi za Rais Dkt Jaliohn Pombe Magufuli za elimu bure.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.