Sunday, August 18

ABDUL NONDO YEYE NA MASOMO BASI TENA

0

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemsimamisha kuendelea na masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul Nondo baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), amesimamishwa kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye

Akizungumza leo na Mwananchi Machi 27, 2018, Profesa Anangisye amesema, “ni kweli barua ya kumsimamisha ni yangu na tumefanya hivyo kwa mujibu wa tararibu zetu

Profesa Anangisye amesema mwanafunzi anapokuwa amepandishwa kizimbani na akawa na kesi ya kujibu husimamishwa na akishamaliza kesi yake anarejea kuendelea na masomo

Wakili wa mwanafunzi huyo, Jebra Kambole amesema kuwa mpaka sasa mteja wake hajapata barua hiyo

“Hatujaipata na hata Nondo mwenyewe pia hajaipata na wala hatujui chochote kuhusu suala hilo hivyo siwezi kusema kama ni ya kweli au ndio mambo ya kwenye mitandao. Ila pia kama ni kweli kwanini isambae mitandaoni, inapaswa apewe mwanafunzi mwenyewe,” amesemaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.