Sunday, August 25

Rais Pierre Nkurunziza Wa Burundi Ametangaza Tarehe Ya Kufanyika Kura Ya Maoni

0


Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametangaza Mei 17 mwaka huu kuwa tarehe ya kufanyika kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba ambayo huenda yakamfanya kusalia madarakani hadi mwaka 2034. Mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yanajumuisha kurefusha muhula wa urais kuongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.

Agizo hilo la rais linakuja siku chache baada ya chama tawala cha Burundi, CNDD-FDD, kumtangaza Nkurunziza kuwa kiongozi wao wa kudumu. Upinzani na makundi ya kutetea haki za binadamu wameitaja kura hiyo ya maoni kuwa njama ya Nkurunziza kusalia madarakani milele. Muhula wa Nkurunziza unapaswa kukamilika 2020. Katibu mkuu wa zamani wa CNDD-FDD, Hussein Rajabu, amesema kura hiyo ya maoni itawagawanya Warundi hata zaidi.

 

Chanzo: DW UjerumaniRead More

Share.

About Author

Comments are closed.