Wednesday, August 21

Mabalozi Wawili Waapishwa Leo Ikulu Jijini Dar es salaam

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Meja Jenerali mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi na IGP-Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018. Rais  Dkt. John Pombe Magufuli pia aliwakabidhi vitendea kazi Mabalozi  Wateule.

Hafla hiyo pia  iliudhuliwa na  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan,  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi balozi John Kijazi Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Ramadhani Mwinyi pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi na Usalama

 

 

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.