Thursday, August 22

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA KAMPALA, APIGWA NA BUTWAA!

0


Dar es Salaam. Asubuhi ya leo Jumanne Februari 20, 2018, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya ziara ya kushtukiza katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala kilichopo maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake hiyo, Ndalichako amepokelewa na wanafunzi huku uongozi wa chuo hicho ukijitokeza dakika chache baadaye baada ya waziri huyo mwenye dhamana ya elimu hapa nchini kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Waziri Ndalichako ameonyesha kusikitishwa kwake na wanafunzi wa chuo hicho kutowatambua kwa majina viongozi wa chuo, na kusisitiza kuwa wanao wajibu wakuwafahamu viongozi wao.

“baada ya kufanyiwa usajili (registration) siuwa mnafanyiwa kozi ya utambulisho wa mazingira na viongozi? Kwanini hamuwajui viongozi wenu? Hamkutambulishwa?” alionyesha kusikitishwa.

Baada ya kufika chuoni na kupokelewa na wanafunzi hao, Ndalichako aliwauliza majina ya mkuu wa chuo,  makamu mkuu wa chuo, na makamu mkuu wa chuo taaluma, maswali ambayo yalishindwa kujibiwa na wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza kwa madai kuwa hawawafahamu viongozi wakuu wa chuo hicho.

Katika hatua nyingine, waziri Ndalichako amekagua miundombinu mbalimbali ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na maabara na kujionea utendaji kazi wa vifaa katika maabara za chuo, pamoja na kusikiliza changamoto kadhaa zilizopo chuoni hapo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.