Monday, August 19

“ULINZI NA USALAMA UMEIMARISHWA SIKUKUU YA PASAKA”, KAMANDA MAMBOSASA.

0


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa ulinzi na usalama katika maeneo yote ya jiji umeimarishwa katika kipindi hiki cha sikuuu ya Pasaka.

Hayo yamesemwa leo Machi 30, 2018, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Amesema jeshi la polisi litakuwa likifanya doria maeneo yote ya jiji, huku akiwataka watumiaji wote wa barabara kuzingatia alama za barabarani wakati wote ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Kamanda Mambosasa pia amepiga marufuku disko toto katika kipindi hiki cha sikukuu, ambapo amesema hawajapata ombi lolote toka kwa wamiliki wa kumbi hizo za watoto, linalowataka kwenda kukagua na kuthibitisha kama ni salama kwa watoto, na hivyo kusisitiza kuwa hakuna ukumbi kwa ajili ya disko toto uliosajiliwa kwaajili ya kutumika na watoto.

Mambosasa pia ametumia fursa hiyo kuwatakia wakazi wa Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla, sikukuu njema ya Pasaka, na kusisitiza washerekee kwa amani na utulivu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.