Wednesday, August 21

NI PATASHIKA STAND UNITED VS NJOMBE MJI, FA CUP LEO.

0


Kikosi cha Stand United

Shinyanga. Robo fainali ya kwanza ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), itaanza kupigwa leo kwenye dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga, ikiwakutanisha wapiga debe wa Stand United dhidi ya wabishi Njombe Mji, kutoka mkoani Njombe.

Kikosi cha Stand United

Mchezo huo utaanza kupigwa mishale ya saa 10:00 jioni, ambapo kila timu itahakikisha inapambana kufa kupona ili iweze kufuzu hatua ya nusu fainali, ambapo mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar.

Kikosi cha Njombe Mji kikiwa mazoezini

Mechi zingine za Robo fainali zitachezwa  siku ya kesho na kesho kutwa kwenye viwanja vya Nafua mkoani Singida, Azam Complex jijini Dar es Salaam, na Sokoine mkoani Mbeya.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.