Friday, August 23

MIGUNA ASAFIRISHWA KWENDA DUBAI CHINI YA ULINZI MKALI, ATUMA UJUMBE MZITO ASUBUHI YA LEO.

0


Wakili Miguna.

Nairobi. Wakili na mwanasiasa wa Kenya aliyeidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raia Odinga kuwa ‘Rais wa Wananchi’, Miguna Miguna amesafirishwa kwa lazima na serikali ya Kenya kwenda Dubai.

Miguna alisafirishwa usiku wa jana Machi 28, 2018, kwa usafiri wa ndege ya shirika la Emirates akiwa chini ya uangalizi wa afisa wa idara ya ujasusi, na ambapo kuna taarifa kuwa kuna mpango wa kumsafirisha tena kutoka Dubai kwenda London, Uingereza.

Mapema asubuhi hii, Miguna ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, ameamka na kujikuta yuko Dubai, na kwamba hali yake ya kiafya sio nzuri na anahitaji matibabu ya haraka.

Kabla ya kusafirishwa kwenda Dubai, Miguna alikuwa amezuiwa kwenye uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa muda wa siku tatu toka siku ya Jumatatu aliporejea akitokea nchini Canada ambako alikuwa huko toka mwezi Februari kufuatia serikali ya Kenya kumtimua nchini kwa lazima.

Ujumbe alioandika wakili MigunaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.