Wednesday, August 21

JESHI LA POLISI LAWASHUKURU WANANCHI KWA USHIRIKIANO, LAWAHAKIKISHIA ULINZI KIPINDI HIKI CHA PASAKA.

0


Dar es Salaam. Jeshi la polisi nchini limesema linawashukuru wananchi ambao wameendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kusaidia kupunguza vitendo vya uhalifu ambavyo vilikuwa vimeshamiri katika siku za nyuma.

Hayo yamesemwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa siku ya jana Machi 28, 2018, ambapo pia alielezea hali ya usalama nchini kuwa ni shwari.

Inspekta Sirro amesema jeshi la polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi wake kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu ya pasaka inasherekewa kwa amani na utulivu, na hakuna vitendo vyovyote vya kihalifu vitakavyofanyika.

Inspekta Sirro amewata pia wazazi kuhakikisha wanawaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na ulinzi wa karibu. Amewataka pia watumiaji wote wa barabara kuhakikisha kuwa wanakuwa makini na kuzingatia sheria zote za barabarani.

Katika kipindi cha sikukuu, matukio mengi ya kihalifu, na ajali za barabarani zimekuwa zikiripotiwa katika maeneo mengi ya nchi, hivyo taarifa hii ya Inspekta Sirro, inatoa faraja kwa watanzania wote ambao wamekuwa wakikemea vitendo vya uhalifu na matumizi mabaya ya barabara ambayo yamekuwa yakisababisha ajali zisizo za lazima.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.