Thursday, August 22

EDEN HAZARD: MIMI SI ZAIDI YA MESSI.

0


London. Kiungo wa kati raia wa Ubelgiji anayekipiga katika klabu ya Chelsea ya England, Eden Hazard, amesema yeye bado hajafikia kiwango cha Muargentina, Liones Messi, anayekipiga katika klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.

kwa mujibu wa habari iliyoripotiwa na BBC, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa yeye amekuwa hafungi mabao mengi kama anavyofanya mchezaji Messi, na hivyo kuwataka mashabiki wa soka kutomfananisha yeye na Messi.

Aidha, akizungumzia mkataba wake unaoelekea ukingoni katika klabu yake ya Chelsea, Hazard amesema kwasasa kipaumbele chake kipo kwenye timu yake ya taifa ambayo inajiandaa na michuano ya kombe la dunia itakayoanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi Juni huko nchini Urusi, na hivyo kusema hayuko tayari kuzungumzia mkataba huo hadi pale michuano ya kombe la dunia itapomalizika.

kwa siku za hivi karibuni mashabiki wa soka hususani barani Ulaya wamekuwa wakifananisha kiwango cha mchezaji huyo na mchezaji wa Barcelona Lionel Messi, kutokana na wachezaji hawa kuwa na uwezo unaofanana wakulimiliki dimba na kuwa na vionjo vingi wawapo uwanjani.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.