Thursday, August 22

TAIFA STARS YAWAZAWADIA WATANZANIA ZAWADI YA PASAKA

0


Wakati tukielekea katika sikukuu za Pasaka Timu ya Taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars jioni imewazawadia Watanzania zawadi ya Pasaka baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya timu ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo maarufu kama The Leopards

Kazi nzuri iliyofanyika kipindi cha pili Kwa vijana wa Tanzania ndiyo iliyowalowesha Congo huku Mbwana Samata na Shiza Ramadhani Kichuya wakipeleka msiba huo Kwa Congo.

Samata alitangulia kuipatia Taifa Stars bao la kwanza dakika ya 74 akiunganisha mpira wa krosi ya Shiza Kichuya na Samata kufunga Kwa kichwa na dakika 10 baada ya bao Hilo Mbwana Samata alifanikiwa kumtengenezea Shiza Kichuya aliyepiga kombora Kali la mita zaidi ya 20 na kumshinda kipa wa Congo.

Matokeo hayo katika mpambano huo wa kimataifa wa kirafiki unaiweka Tanzania pazuri hasa katika viwango vya Soka duniani ikizangatia Congo wanashika  nafasi ya tatu katika ubora barani Afrika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.