Wednesday, August 21

SINGIDA UNITED: YAKANUSHWA KUFUNGIWA KWA DANNY LYANGA

0


Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Mkurugenzi mkuu Festo Sanga umekanusha taarifa za kufungiwa kwa mshambuliaji wao Daniel Lyanga na shirikisho la soka Duniani FIFA kwa madai ya kusaini mkataba na timu mbili.


Sanga amesema anashangaa kusikia taarifa hizo bila uongozi wao kuulizwa ni nini chanzo kilichomfanya Lyanga asiweze kucheza katika michuano ya ligi kuu na Azam Sports Federation Cup toka asajiliwe katika dirisha dogo Disemba mwaka jana.

Sanga amesema ukweli wa jambo hilo ni kuwa Lyanga alisajiliwa katika dakika za mwisho kabisa Kabla ya dirisha la usajili kufungwa kwa makubaliano na klabu ya Fanja ya Oman lakini cheti cha uhamisho (ITC)’ ndicho kilichochelewa.

Lyanga alipewa barua ya kuachwa na klabu yakye ya Fanja wakati wakitaka kumsajil, taarifa kuwa Danny lyanga amefungiwa sio kweli.

Asubuhi ya leo kumezuka taarifa ya kuwa Daniel Lyanga amefungiwa miezi sita na FIFA kwa kusaini mkataba na timu mbili tofauti Fanja FC ya Oman na Singida United ya Tanzania.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.