Thursday, August 22

RONALDO AJIWEKEA REKODI NYINGINE URENO

0
Mchezaji bora wa soka duniani na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana alijiwekea rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza anayeendelea kucheza soka mwenye mabao mengi zaidi katika timu yake ya Taifa akifunga mabao yaliyoiwezesha Ureno kushinda bao 2-1 dhidi ya Misri.

Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ulikuwa moja kati ya michezo mingi iliyopigwa jana katika mwendelezo wa mechi za kimataifa za kirafiki katika kalenda ya FIFA.

Mpaka dakika ya 90 Ureno walikua nyuma Kwa bao 1-0 dhidi ya Mafarao hao wa Misri goli lililofungwa na Mohamed Salah dakika ya 56 na wengi wakiamini kama mchezo huo ungeisha hivyo ndipo Ronaldo alipofanya yake

 90’+2 Cristiano Ronaldo
 90’+4 Cristiano Ronaldo

Baada ya kufunga magoli hayo Ronaldo sasa amefikisha magoli 81 akiwa na timu yake ya Taifa akishika  nafasi ya kwanza kati ya wachezaji waliofunga mabao mengi wanaoendelea kuzichezea timu zao za taifa na amekuwa mchezaji wa tatu katika orodha ya wachezaji wa muda wote walioweza kufunga mabao mengi wakiwa na timu zao za Taifa.
Ali Daei (Mchezaji wa zamani wa Iran)

ORODHA YA WAFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE
– Ali Daei (Mchezaji wa zamani wa Iran) – 109
– Ferenc Puskas (Mchezaji wa zamani wa Hungary) – 84
– Cristiano Ronaldo  (Nahodha wa sasa wa Ureno) – 81

Ronaldo bado Ana nafasi ya kuweza kuwapiku Ali Daei anayeongoza orodha hiyo pia nafasi iko wazi  kuweza kumzidi Puskas anayeshika nafasi ya pili.
Ikumbukwe…
Tarehe 12 Juni 2004 Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la kwanza akiichezea Ureno na  jana tarehe 23 Machi 2018 amefunga bao la 80 na 81 akiwa na Ureno.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.