Sunday, August 18

MMESIKIA BALAA LA RONALDO HUKO LA LIGA? APIGA 4 REAL IKIUA 6

0Real Madrid 6-3 Girona: Cristiano Ronaldo hat-trick in thriller
Mchezaji bora wa dunia na mshambuliaji wa Real madrid Cristiano Ronaldo jana alifunga mabao manne katika ushindi wa bao 6-3 walioupata Real Madrid Nyumbani dhidi ya Girona

Ronaldo ambaye magoli yake manne ya jana yamemfanya kufikisha magoli 22 msimu huu akiwa ni wa pili katika orodha ya wafungaji bora wa La Liga akiwa nyuma ya Messi mwenye magoli 25 akifikisha pia hat-trick yake ya 50 katika mashindano yote tangu alipoanza kucheza soka la ushindani.

Ronaldo alifunga mabao yake dakika ya 11,47,64 na 90 huku gareth Bale na Lucas Vazquez wakifunga bao moja kila mmoja wakati Cristian Stuani aliifungia Girona mabao mawili na Juanpe akafunga bao moja.

Real Madrid kwa ushindi huo imefikisha pointi 60 katika nafasi ya tatu huku Barcelona ambao jana waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Atletico Bilbao wakiongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 75 huku Atletico Madrid wao ambao jana walifungwa bao 2-1 na Villareal wakishika nafasi ya pili na pointi zao 64Read More

Share.

About Author

Comments are closed.