Saturday, August 17

LICHA YA KUTOKA SARE, YANGA YASONGA MBELE MABINGWA AFRIKA.

0


Wawakilishi wa Tanzania bara kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika Yanga wameweza kutinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Mabingwa wa Sheli Sheli St. Louis.

Mchezo huo wa marudiano wa hatua ya awali ya michuano hiyo mikubwa katika ngazi ya klabu ulichezwa jioni hii katika mji mkuu wa Sheli Sheli Victoria.

Ibrahim Ajibu ndiye aliyefunga bao la kuongoza Kwa Yanga katika kipindi cha kwanza bao ambalo lilidumu mpaka dakika 90 kabla ya Wenyeji hawajapata bao la kusawazisha muda wa nyongeza.

Yanga imevuka hatua hii baada ya ushindi wake wa bao 1-0 nyumbani wiki moja iliyopita ambao inawafanya  kusonga mbele Kwa ushindi wa jumla wa bao 2-1.

Matokeo hayo sasa yanawafanya Yanga kutinga hatua ya kwanza ambapo watakutana na Mshindi wa mechi baina ya Township Rollers ya Botswana au El Merrekh ya Sudan.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.