Saturday, August 17

KICHUYA: BADO HATUJAMALIZA KAZI KWA GENDARMERIE

0


Winga wa timu ya Simba, Shiza Kichuya amekiri kuwa bado wana kazi kubwa kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Djibouti licha ya ushindi mnono waliopata kwenye mechi ya awali.

Kichuya ambaye ndio michuano yake ya kwanza ya Afrika amesema wanatarajia kupata upinzani mkubwa kuliko ilivyokuwa mchezo wa kwanza walioibuka na ushindi wa mabao 4-0 jijini Dar es Salaam.

Winga huyo aliyasema hayo muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea nchini Djibouti akiwa na wachezaji wenzake na benchi la ufundi kwa ajili ya mchezo wa maruadiano utakaopigwa siku ya Jumatano.

Kichuya ambaye anatarajia kuwa miongoni mwa nyota 11 wa Simba watakaonza mchezo huo amesema lolote linaweza kutokea hivyo wataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa.

“Bado hautajamaliza kazi kuna dakika 90 nyingine Djibouti kwahiyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda tena,” alisema Kichuya.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.