Thursday, July 18

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA KAMPENI YA KUCHANGIA TIMU YA TAIFA ‘TAIFA STARS’

0


Katibu wa Kamati ya kuisadia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Mhandisi Hersi Said (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa harambee maalum ya kuichangia timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Paul Makonda.

Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda akimkaribisha Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Mbunifu wa mavazi akionesha kwa waandishi wa habari vazi maalum kwa ajili ya washangiliaji wa timu ya Taifa “Taifa Stars”, inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda (katikati) akijaribu vazi maalum kwa ajili ya washangiliaji na mashabiki wa timu ya Taifa “Taifa Stars”, inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu toka kushoto) akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha kufuzu kwa timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Picha na WHUSM – Dar es Salaam.

Share.

About Author

Leave A Reply