Monday, August 26

SERIKALI YATOA TAMKO KWA WATU WENYE VITAMBI TANZANIA

0Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema uwepo wa vitambi ni mojawapo ya dalili za mtu ananyemelewa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza na kuwataka watu wenye vitambi kuzingatia suala la mlo bora.

Naibu Waziri Ulega ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali kwa niaba ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambapo amesema si dalili nzuri.

Akizungumza kwenye kikao hicho Naibu Waziri Ulega amesema kuwa “kitambi ni dalili mojawapo ya uzito kupita kiasi hii si dalili njema, hupelekea magonjwa yasiyoambukiza”

Aidha Naibu Waziri Ulega amesema kuwa “katika kupambana na kitambi nikujikinga kupunguza chakula cha wanga, sukari, chumvi, mafuta kwenye chakula, kunywa maji lita 1 na nusu na kupunguza unywaji wa pombe uliopitiliza”

Kwa sasa Bunge linaendelea Bungeni jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply