Wednesday, July 17

RAIS MUSEVENI WA UGANDA KUTUA KESHO KWA RAIS DKT. MAGUFULI CHATO

0


Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kesho Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019 atafanya Ziara Binafsi ya siku 1 moja hapa nchini.


Mhe. Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.


Akiwa Chato, Mhe. Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

12 Julai, 2019

Share.

About Author

Leave A Reply