Tuesday, August 20

MTOTO MCHANGA ALIYEZIKWA HAI AOKOLEWA NA MBWA

0


MTOTO MCHANGA ALIYEZIKWA HAI AOKOLEWA NA MBWA – MWANAHARAKATI MZALENDO ™

New

Mbwa mmoja nchini kaskazini mwa Thailand amemuokoa mtoto mchanga aliyekuwa amezaliwa baada ya kuzikwa hai anayedaiwa kuzikwa na mwanamke mwenye umri mdogo.

Mwili wa mtoto huyo mchanga wa kiume unasemekana ulikuwa umezikwa na mama mwenye umri wa miaka , 15, ambaye alikuwa amewaficha wazazi wake ujauzito.


Mbwa kwa jina Ping Pong alionekana akiwa anabweka na kuchimba ardhini kwenye shamba katika kijiji cha Ban Nong Kham.


Mmiliki wake anasema aliposogelea mahali alipokuwa ndipo alipoona mguu wa mtoto mchanga ukitokezea juu ya ardhi.


Wanakijiji walimkimbiza mtoto hospitalini ambako madaktari walimuogesha na kutangaza kuwa alikuwa mzima wa afya.


Mmiliki wa mbwa Ping Pong , Usa Nisaikha, anasema mguu wa mbwa hake hauna nguvu baada ya kugongwa na gari.


Aliliambia gazeti la Khaosod : ” Ninamtunza kwasababu ni mwaminifu sanana kila mara huwa ananisaidia ninapokwenda shambani kuwahudumia mifugo wangu. Anapendwa sana na kijiji kizima.


Inashangaza.”


Mama yake mtoto huyo mchanga amekwishashtakiwa kwa kumtelekeza na kujaribu kumuua.


Panuwat Puttakam, afisa lkatika kituo cha Chum Phuang, alililiambia gazeti la the Bangkok Post kuwa sasa mama huyo anahudumiwa na wazazi wake pamoja na mtaalamu wa kisaikolojia.


Alisema anajutia matendo yake.


Wazazi wa msichana wameamua kumlea mjukuu wao.


Share.

About Author

Leave A Reply