Wednesday, August 21

Makonda atangaza vita na Wamachinga wasio na vitambulisho Dar

0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuanzia June 3 mwaka 2019 ni marufuku kwa Wamachinga wote wasio na vitambulisho kufanya biashara katika maeneo yote jijini Dar.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 29, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mwitikio wa wafanyabiashara kuchukua vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais John Magufuli kwa wakuu wote wa Mikoa nchini.

Makonda amesema Jiji hilo lilipatiwa vitambulisho 175,000 lakini wapo ambao hawajachukua hadi sasa.

Amesema kuwa atafanya msako mkali kuwatafuta wamachinga
wote wasio na vitambulisho hivyo

Advertisement

==

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==

….

===

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Share.

About Author

Leave A Reply