Wednesday, August 21

Linah Afungukia Kutaka Mtoto Mwingine

0


Linah, ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Tracey, amefunguka kuwa moja ya mipango yake kwa sasa ni kuwa na mtoto mwingine na mwanaume ambaye yupo naye kwa sasa.

Najua watu wengi wanahoji mahusiano yangu ya sasa, lakini wanatakiwa kufahamu na mimi natakiwa kuwa na mambo binafsi, kwa sasa mipango yangu ni kuwa na mtoto na haijalishi atakuwa wa baba yupi, kikubwa ni mimi kuridhika na mtu ambaye natamani kuwa naye na kupata mtoto,î alisema Linah.

Kwa sasa Linah anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na aliyekuwa mpenzi wake wa awali, Amini, ambaye kwa sasa wametoa ngoma mpya.

‘Nimenasaí, inayofanya vizuri sehemu mbalimbali.

Share.

About Author

Leave A Reply