Thursday, August 22

Waziri Ndalichako Atishia Kukifunga Chuo cha Mount Meru

0


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof.  Joyce Ndalichako amekitaka Chuo Kikuu cha Mount Meru kilichopo Jijini Arusha kuacha mara moja utaratibu wa kutoa alama za makisio kwa Wanafunzi wanosoma chuoni hapo na wakiendelea Serikali itakifunga chuo hicho mara moja kwa sababu utaratibu huo haujawahi kutumika katika Chuo chochote Duniani.

Waziri Ndalichako ametoa maagizo hayo alipotembelea katika Chuo hicho kuona miundo mbinu na namna wanavyo simamia utoaji wa elimu ya juu, ambapo amesema Wizara ilishatoa maelekezo kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kuwa Chuo hicho kiwaondoe Wahadhiri ambao hawana sifa za kufundisha lakini agizo hilo mpka sasa halijatekelezwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.