Sunday, August 25

Waziri Mkuu Afunguka Kuhusu Wizara Kukosa Majina

0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ofisi mpya za wizara saba katika mji wa Serikali ulioko Mtumba, Dodoma na kusisitiza uwekwaji wa vibao vya ofisi na kukamilisha mazingira ya nje.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akitoa majumuisho ya ziara fupi kwa maafisa wa Serikali waliokuwepo kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati.

Waziri Mkuu amesema, “kuna wizara hazina majina kwa nje, hakikisheni majengo yote yanawekwa majina haraka ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaokuja huku kutafuta huduma, nia ya Serikali ni kutoa huduma zote kutokea hapa Mtumba.”

“Nimefurahi kukuta Mawaziri, Naibu wao na Makatibu Wakuu pamoja na wakuu wa idara wako huku na kazi zinaendelea, lakini ni lazima nisisitize kwamba idara zinazohamia huku ziwe ni zile zenye kutoa huduma za kila siku kwa wananchi,” amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu ameongeza “ni lazima tuwaeleze wananchi na wadau wetu ili watambue kwamba Serikali imehamia huku, lakini wakija kutaka huduma wasikute idara inayowahusu iko mjini au wengine wako huku na wengune wako kule.”

Share.

About Author

Leave A Reply