Friday, August 23

Waliouawa Kwenye Mashambulio ya Makanisa na Hotel Sri Lanka Wafikia 290

0


Idadi ya watu waliouawa kwenye mashambulio ya mabomu kwenye makanisa na hoteli nchin Sri Lanka imepaa na kufikia 290.

Milipuko nane iliripotiwa jana Jumapili katika mashambulio yaliyolenga makanisa matatu mjini Kochchikade, Negombo na Batticaloa ambayo yalisahambuliwa wakati wa ibada ya Pasaka.

Hoteli za The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury ambazo zipo mjini Colombo, pia zilishambuliwa.

Watu wengine zaidi ya 500, wamejeruhiwa na kuna hofu idadi ya vifo ikaendelea kuongezeka.

Jumapili ya Pasaka ni moja ya siku kuu muhimu sana katika kalenda ya waumini wa dini ya Kikristo.

Hakuna kundi lolote lililojihusisha na mashambulizi hayo. Lakii ni dhahiri washambuliaji walilenga siku hiyo ili kuumiza watu wengi kadri iwezekanavyo.

Kumekuwa na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka masariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.

Watu 24 wamekamatwa kufikia sasa wakihusishwa na shambulio hilo.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumapili jioni, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ranil Wickremesinghe alizungumzia uvumi kuwa maafisa usalama walikuwa na fununu za kiintelijensia juu ya uwezekano wa kutokea mashambulo.

“Lazima yuangalie ni kwanini hatua stahiki hazikuchukuliwa ili kuzuia mashambulizi hayo. Si mimi wala mawaziri wengine ambao walitaarifiwa juu ya uwepo wa taarifa hizo za kiintelijensia awali,” amesema Wickremesinghe.

“Kwa sasa kipaumbele ni kuwatia nguvuni wale waliotekeleza mashambulizi hayo,” ameongeza.

Bomu lilipuka wakati vikosi maalum vikifanya msako katika nyumba moja karibu na mji wa Colombo
Amri ya kutotoka nje imewekwa kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Sri Lanka (12:30-00:30 GMT).

Serikali pia ilidhibiti matumizi ya mitandao yote ya kijamii kwa muda ili kuzuia taarifa potofu kuenezwa.

Kanisa la St Sebastian mjini Negombo limeharibiwa vibaya na milipuko hiyo.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha paa la jengo la kanisa lililoharibiwa vibaya huku damu ikiwa imetapakaa ndani ya kanisa.

Karibu watu 67 wameripotiwa kufariki ndani ya kanisa hilo.

Share.

About Author

Leave A Reply