Tuesday, August 20

Viongozi wa MDC-T Wavurugana Mazikoni kwa Tsvangirai

0


Viongozi wa MDC-T Wavurugana Mazikoni kwa Tsvangirai

Makamu wa Rais wa MDC-T Thokozani Khuphe, Katibu Mkuu Douglas Mwonzora na mratibu wa kitaifa, Abednico Bhebhe Jumanne walilazimika kujificha kwenye kibanda cha Waziri Mkuu wa zamani, Morgan Tsvangirai kukimbia vita vya madaraka ya chama.

Khuphe na Mwonzora wako upande ambao unapingana na upande wa kaimu kiongozi wa MDC-T Nelson Chamisa ambaye alitwaa madaraka saa chache baada ya kutangazwa kuwa Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa kansa ya utumbo.

Washambuliaji walimsakama Khuphe mara alipofika kwa ajili ya mazishi. Alipoonekana tu akishuka kwenye gari lake huku akiwa ameongozana na walinzi wawili na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwa Tsvangirai, kundi la watu lilimfuata mwanamama huyo na kuanza kumsakama.

Naibu waziri mkuu wa zamani alikimbia kuokoa maisha yake kwa kuingia nyumba ya jirani huku akifuatwa na kundi la watu. Baadaye aliokolewa na walinzi wa ZRP.

Khuphe alionekana akitetemeka na akitokwa machozi muda wote wakati Mwonzora alionekana dhahiri amefura kwa hasira. Bhebhe alichukua jukumu la kuwa mratibu na alionekana kuikubali hali hiyo.

Shuhuda mmoja alieleza hali ya kutisha wakati Khuphe na Mwonzora wakishambuliwa kwa maneno kabla ya kuingia ndani ya nyumba ya mmoja wa majirani wa Tsvangirai.

“Kundi la zaidi ya watu mia moja lilitumia mawe na fimbo kuwashambulia. Mwanamke mmoja (Lwazi Sibanda) alipigwa na chupa tupu ya bia na akawa anavuja damu.

“Walitishia kuchoma nyumba hiyo na wakatupa mawe kupitia dirisha kwa jitihada za kumpiga Khuphe,” shuhuda aliliambia New Zimbabwe.

Mwonzora alithibitisha kuwa walishambuliwa, akimshutumu Chamisa kuwa nyuma ya vurugu.

“Mwanzoni watu 10 walitushambulia, lakini maofisa usalama waliwamudu. Wakaenda kuongeza nguvu na kurudi wakiwa zaidi ya 100,” alisema.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.