Thursday, August 22

Ugonjwa wa Dengue umerejea nchini baada ya wagonjwa 11 kugundulika katika Hospitali ya Ocean Road

0DAR: Ugonjwa wa Dengue umerejea nchini baada ya wagonjwa 11 kugundulika katika Hospitali ya Ocean Road

Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imeeleza kuwa homa ya ugonjwa huo imendulika baada ya wagonjwa kadhaa waliokuwa na dalili zake kupimwa na kuthibitishwa

Mara ya kwanza ugonjwa huo uligundulika mwaka 2014 ambapo wagonjwa 400 waliupata. Walitibiwa na kupona, isipokuwa watatu ndiyo walifariki dunia

Tahadhari imetolewa kwa wananchi kupima afya haraka wanapohisi wana homa Kali, mafua na kuumwa kichwa kwa muda, ambazo ni dalili kubwa za homa ya dengue

Vimelea vya ugonjwa wa homa ya dengue husambazwa na mbu kama ilivyo kwa malaria. Hivyo wananchi wanahimizwa kuua mazalia ya wadudu hao harakaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.