Wednesday, May 22

Timu ya Taifa Stars Yawaomba Radhi Watanzania Baada ya Kufungwa

0


Timu ya Taifa Stars Yawaomba Radhi Watanzania Baada ya Kufungwa

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeomba radhi kwa mashabiki kWA kupoteza mchezo wao wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika Camerooni.

Stars walikuwa kwenye nafasi nzuri endapo wangeshinda wangefanikiwa kufuzu moja kwa moja ila kwa kuwa walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 watalazimika kusubiri mpaka mwakani baada ya mechi za mwisho kuchezwa.

Beki wa kulia wa Stars, Erasto Nyoni amesema kuwa wanatambua wamepoteza furaha ya mashabiki hivyo wanaomba msamaha kwa kufanya hivyo kwani walipambana wakashindwa kupata matokeo.

“Hakuna ambaye amefurahi kushindwa hasa kwa kuwa taifa lilituamini na tuliahidi kufa na kupona ili tuweze kupata matokeo ila tumepoteza bado tunaamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa mwisho, kikubwa sapoti watanzania msituache,” alisema.

Kwenye Kundi L timu ya Uganda imefanikiwa kufuzu Fainali hizo huku ushindani ukibaki kwa timu mbili ambazo ni Tanzania na Lesotho wakiwa na pointi 5, matumaini yatajulikana mwezi Machi kwa timu ya Tanzania kama watashinda  dhidi ya Uganda huku Lesotho wakipoteza kwa Cape Verde.

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply