Sunday, August 18

SUGU "Mimi ni Wale Tunaomuunga Mkono Rais Magufuli Bila Kuhama Chama" _

0


Mbunge wa Mbeya wa Mjini Joseph Mbilinyi amesema yeye ni miongoni mwa Wabunge ambao wanamuunga mkono Rais Magufuli licha ya kutohama chama na amedai ataendelea kumuunga mkono hadi mwisho.

Mbunge Sugu ametoa kauli hiyo katika ziara ya Rais Magufuli, alipozindua kiwanja cha Ruwanda Nzovwe Mkoani Mbeya ambapo alipata nafasi ya kuhutubia kwenye mkutano huo wa hadhara. “Mimi ni katika watu tunaokuunga mkono bila kuhama chama, na nitaendelea kukuunga mkono mpaka mwisho, wanasema kuna watu wamepanga kufanya fujo, haiwezekani watu na akili zao wapange kumfanyia fujo Rais,” amesema Mbunge Sugu.

Akimzungumzia Mbunge huyo, Rais Magufuli amesema kuwa, “asanteni kwa mapokezi mazuri sana hata Mbunge wa hapa ndugu Sugu naye alisugua hadi Airport kuja kunipokea na akanisindikiza hadi nilipoenda sijui ndiyo muelekeo wa CCM.

Share.

About Author

Leave A Reply