Sunday, December 16

Sababu za Rais kutopewa hela hadharani

0


Sababu za Rais kutopewa hela hadharani

Huenda ukawa unajiuliza kama kuna mipaka yeyote juu ya upokeaji wa zawadi yeyote kwa watumishi wa Umma, ndiyo maana ni mara chache kuonekana hadharani wakipewa zawadi, kama pongezi binafsi au kwa majukumu aliyoyafanya.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Mungano Tanzania ya mwaka 1977, Rais wa Tanzania ndiye kiongozi mkuu wa watumishi wa umma nchini ndiyo maana hata wizara husika inayoongozwa na Waziri George Mkuchika iko chini ya Ofisi yake kama Wizara ya nchi ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.

Kitu pekee kinachowafanya viongozi mbalimbali kuonekana kutopewa zawadi au pongezi ya fedha kwa kutimiza majukumu yake binafsi ni sheria ya maadili ya viongozi wa Umma namba 13, ya mwaka 1995 kifungu cha 12 kinachozungumzia marufuku ya kiongozi wa umma kujinufaisha kifedha.

Kifungu hicho cha 12, sehemu ya 2 inaeleza “kiongozi wa umma pale atakapo pokea zawadi yenye thamani ya zaidi shilingi elfu 50, atalazimika kuitaja aina ya zawadi na thamani ya zawadi hiyo” aidha sehemu 2(b) inamtaka kiongozi wa umma atakayepokea zawadi yenye thamani ya zaidi shilingi elfu 50, kuikabidhi kwa afisa muhasibu wa ofisi inayohusika.

Aidha sehemu 2(b) imeeleza “Afisa Muhasibu atalazimika kutoa maagizo kwa maandishi matumizi ya zawadi hiyo au jinsi ya kuishughulikia kwa njia nyingine yeyote.”

Katika kuhakikisha viongozi wa umma wanakuwa na maadili wamekuwa wakilazimika kujaza fomu maalum kwa ajili ya tamko la rasilimali, ili kufahamu mali zinazomilikiwa na viongozi wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, na Wakuu wa wilaya.

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply