Monday, August 26

Rais Apiga Marufuku Picha yake Kuwekwa Kwenye Maofisi

0


Rais mpya wa Ukraine, Volodymyr Oleksandrovych Zelensky amepiga marufuku picha yake kuwekwa kwenye ofisi za umma kwa kile alichodai kuwa Urais sio umaarufu

Rais Zelensky amesema kuwa badala ya kuwekwa picha zake ukutani, kila mmoja aweke picha ya watoto wake ili awe anaitazama kila anapofanya maamuzi kwa ajili ya nchi

Zelensky aliyekuwa msanii maarufu wa vichekesho alishinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika April 21 mwaka huu

Share.

About Author

Leave A Reply