Saturday, August 24

Pogba kuitema Manchester United siri yafichuka

0


Imebainika kuwa wakala Mino Raiola ndio chanzo cha Paul Pogba cha kutaka kuondoka Manchester United.

Staa wa zamani wa Tottenham na timu ya Taifa ya Misri, Ahmed Hossam `Mido’ alisema anafahamu kuwa wakala Raiola ndio anamvuruga Pogba kiasi cha kushikilia kutaka kuondoka msimu huu.

Mido, ambaye alifanya kazi na Raiola kwa kipindi cha miaka 10, alisema anafahamu kuwa Raiola atakuwa bize akisaka timu ya kumnunua Pogba. Manchester United haina mpango wa kumuuza kiungo huyo ingawa kumekuwa na taarifa kuwa Pogba mwenyewe anashinikiza aondoke.

Real Madrid kwa muda mrefu sasa inahusishwa kama timu ambayo inataka kumsajili Pogba na Mido amefichua kuwa wakala huyo atakuwa anafanya mambo yake chini kwa chini.

“Wakala wa Pogba ni Mino Raiola na mimi nimefanya kazi na Mino, ambaye alikuwa wakala wangu kwa miaka 10 kwa hiyo nafahamu vizuri namna anavyofanya kazi,” alisema Mido.

Mido alisema kuwa Raiola atakuwa ameshapiga hesabu zake na kuamini sasa ni wakati muafaka wa kumuuza Pogba.

“Sioni kabisa Pogba akibakia Manchester United lazima Raiola atakuwa anamtafutia timu kwa sasa. Kwa sababu kwa sasa anaona hali ya Manchester United haieleweki,” aliongeza Mido.

Share.

About Author

Leave A Reply