Saturday, August 24

Nimekaria Kufunga Ndoa na Nilimdanganya Mchumba Wangu Kuwa Mimi ni Bikira, Je Nifanyaje?

0


Mwenzenu karibia yananikuta makubwa sijui itakuwaje natamani siku zigande….mimi ni msichana wa miaka 23 nilikutana na Mkaka mmoja mwaka umepita sasa tukawa wachumba akanitambulisha kwao na mie nikamtambulisha kwetu na kuanza uchumba rasmi lakini katika kipindi hicho chote wakati tunaanza nilimdanganya mimi bikira kaka wawatu akafurahi sana na kuahidi kutonigusa mpaka siku ya harusi yetu na kweli kaka wa watu hakunigusa mpaka leo zimebaki week mbili tufunge Harusi..na amewaambia wazazi wake waandae zawadi watakayo nipa baada ya kunitoa bikira siku ya Harusi tutakapofanya kwa mara ya kwanza ,

Eti atawapelekea shuka lenye damu alafu nipewe zawadi ya kujitunza, ki ukweli mimi sina bikira kabisaaa, ilitoka toka na miaka 15 , Naombeni ushauri hili litanitokea puani na kunipa aibu

Share.

About Author

Leave A Reply