Sunday, August 25

Mweyekiti wa Chadema Ahamia CCM

0


 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Chato, Steven Nyororo pamoja na wanachama wengine 200 wamekihama chama hicho na kutangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM kwa kile walichokidai kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Wanachama hao wamepokelewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Idd Kassim Idd ambapo wanachama hao wapya walikula kiapo cha kujiunga na CCM Mkoa wa Geita.

Wanachama  hao wa CHADEMA wilayani Chato pia wamepokelewa na Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Geita, David Azaria, ambapo miongoni mwao pia yupo aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Chato ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Maendeleo Kata ya Buziku.

Wanachama hao wote walikabidhi kadi ya pamoja na uamuzi huo, wananchi wa Kata ya Buziku pamoja na kukabidhi nyaraka mbalimbali za CHADEMA.

Share.

About Author

Leave A Reply