Wednesday, July 17

Mpoki Hamnazo KICHWANI Afunguka "Nikiachana na Mwanamke, Nachukua Kila Kitu Changu"

0


Mchekeshaji maarufu ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni kinachoruka kupitia Radio Efm, Sylvester Mujuni almaarufu Mpoki amesema akiachana na mwanamke ambaye amekuwa naye kwenye mahusiano basi anamnyang’anya vitu vyote alivyomnunulia.

Mpoki amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Block 89 kinachoruka kupitia Radio Wasafi FM na kuongeza kuwa anafanya hivyo ili mwanaume atakayeingia katika mahusiano na mwanamke mwingine naye aanze upya kama yeye alivyomkuta mwanamke huyo.

Majibu yamekuja baada ya kuulizwa kama anayeweza kurudisha fedha ikiwa ametumiwa kwa bahati mbaya na mwanamke aliyeachana naye, ambapo alisisitiza kuwa huwa hana masihara kwenye masuala ya hela.

“Kwanza mimi sijawahi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ananipa hela, sana sana wao ndiyo wanataka kutoka kwangu,” amesema Mpoki.

Kuhusu sababu ya yeye kukubali kuteuliwa kuwa Mshereheshaji wa hafla ya kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mama Diamond na mpenzi wake Diamond, Tanasha Donna, Mpoki amesema ni heshima aliyopewa na Diamond baada ya kumfuata na kumuomba ahodhi tukio hilo kubwa.

Share.

About Author

Leave A Reply