Friday, July 19

Mke Wangu Kanichezea Umafia Huu Baada ya Kutaka Kuchepuka…Kanifuata Mpaka Morogoro

0


Enzi hizo niko na wife. Nishamuaga tangia siku tatu nyuma kua Jumapili nitasafari kikazi kwenda Morogoro kwa muda wa siku tatu. Huku mimi nilikua nishapanga na sweetie wangu Mboni kwamba tunaenda kula bata Morogoro kuanzia hiyo Jumapili hadi jumatano yake! Tukakubalianaa nimpitie kituo cha bus Kimara Baruti

Wife alikua kanifungashia vizuri sana nguo zangu na mahitaji mengine ya safari katika bag langu(wanaume tunadhambi saa zingine!). Na ilipofika muda wa safari akanitaka nimpe lift nimuache salon akatengeneze nywele zake

Tulipofika hapo salon akataka nimsubiri dakika tano tu aangalie kama kuna foleni maana alikua hajawapigia simu, na baada ya muda huo akaja akanambia bado kuna foleni kwahiyo nimpe lift hadi stand ya mkoa kuna parcel katumiwa toka Tanga na mama yake na kashapigiwa simu akaifuate

Nilipofika maeneo ya stand ya mkoa akanambia “Twende hadi TANESCO Ubungo nitashuka nifanye mazoezi ya kutembea, nitarudi kwa miguu hadi stand ya mkoa”. Ile nataka ku park ashuke hapo TANESCO akanikataza akasema “Twende tu nitakwambia nitaposhukia”

Ikabidi ninyooshe tu huku nina wasiwasi kibao nikijiuliza bila majibu nini kinachoendelea! Tulipofika Baruti nikapiga jicho pale kituoni huku kiroho kinanidunda, nikamuona Mboni amekaa pale stand na akawa ameiona gari ila wife hakuonekana kama ameshtukia kitu chochote. Nikaichukua simu yangu nikajifanya kama napiga nikaitoa mlio maana nikahisi Mboni angepiga

Tulipofika Mbezi mwisho nikamwambia wife huoni kua unakuja mbali sana? Akanijibu “Nimekwambia Sesten wee twende nitakapotaka kushuka nitakwambia” Sikumuuliza tena wapi atashuka na huwezi amini tulifika hadi Moro tukaingia Morogoro Hotel kama saa kumi na mbili kasoro hivi

Bahati nzuri kulikua na mabango yanayoonyesha kuna taasisi kadhaa zina semina, workshops na training hapo hotelini na mimi nikambabatiza muhudumu kwa kumwambia kumbe taasisi hii wanafanyia ukumbi wa Chief Kingalu? Wife akasikia nilivyojibiwa “Ndiyo” maana na yeye alishuka kwenye gari na kunifuata counter, kisha tulichukua room

Nikawa kazi yangu tukiamka asubuhi mimi natoka nasema naenda ukumbini kumbe napitiliza hadi town naenda sehemu nyingine kabisaa, tena bila gari huku yeye anabaki hotelini na wakati mwingine anatoka na gari anaenda tu kuzurura mjini. Bahati nzuri nilipo mpigia Mboni na kumweleza yaliyonipata alinielewa akasema “Nilimuona dada kwenye gari ndio maana hata sikupiga simu”
Ilipofika J5 tuka check out na kurudi zetu Dar na wala hakukua na dalili yoyote ya ugomvi, kununiwa au wasiwasi, kitu ambacho kinafanya nijiulize hadi leo kua hivi yule mwanamke alikua anafikiria nini? Alitaka kunifanyia surprise? Alihisi anaibiwa? Au alitakatu kubadilisha location na scene ya kugegedana? Maana sio kwa umafia ule aisee!

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply