Thursday, August 22

Mjadala..Wanaume Wengine Hutongoza Vibaya Hadi Kero

0


Ndani ya JamiiForums katika Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki kuna mada moto za Uhusiano zinajadiliwa, moja wapo inahusu namna Wanawake wanavyochukizwa na namna baadhi ya Wanaume wanavyotongoza

Mdau mmoja anasema anashangazwa na Mwanaume anayemuomba namba ya simu kisha anakuwa anamtumia fedha hata kama hajamuomba. Baada ya siku akiwa hata hajamtongoza anamwambia “Nina hamu nawe tukutane wapi?”

Mdau mwingine anasema anashangazwa na Mwanaume anayekutana naye na kubadilishana naye namba za simu, kisha kupiga stori za kawaida. Siku moja anamuomba kwenda kwake kumsalimia na akifika anataka penzi wakati hajamtongoza

Aidha, Mdau mwingine anasema anachukizwa na Mwanaume ambaye unakuwa rafiki yake na anayependa kukaa naye na kuongea naye lakini bila kumtongoza anaanza kuwaambia watu kuwa “Yule ni demu wangu”


Je, unazungumziaje Wanaume wanaotongoza Wanawake kwa namna hii? 

Share.

About Author

Leave A Reply