Monday, March 18

Kauli ya Shilole kuhusu Chid Benz

0


Mwanadada Shilole amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa iliyomfanya yeye kumshirikisha Chid benz katika wimbo wake mpya ni kwa sababu Chid benz ni msanii kama walivyo wasanii wengine na wala sio vinginevyo. 

Akiulizwa kuhusu baadhi ya wasanii kuwa wakimsema na kumuweka katika makundi mabaya shilole anasema kuwa watu wanatakiwa kuangalia alipotoka Chid Benz na kitu alichowahi kufanya katika muziki wa bongo fleva na sio kumdharau kwa sasa kwa sababu ameshuka. 

watu hawaelewi tu, chid Benz ni msanii mkubwa sana na anapaswa kupewa heshima yake kwa sababu ameweka mchango  mkubwa sana katika kuisimamisha bongo fleva,  kwanini watu wanasema kuwa sio msanii? Na mimi nilimchukua yeye kwa sababu chid ana uwezo wa kuandika ngoma kuliko hata wanavyofikria wao. 

Shilole anakiri kuwa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha Chid Benz yeye hakuiandika bali iliandikwa na Chid Benz mwenyewe. 

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply