Sunday, August 18

Hatujakata Tamaa Tutapambana – Serengeti Boys

0


Hatujakata Tamaa Tutapambana - Serengeti Boys

LICHA ya kupoteza mechi zao mbili walizocheza, kocha wa timu ya Serengeti Boys, Oscar Mirambo amefunguka kwamba bado hawajakata tamaa na watapambana katika mechi yao ya mwisho mbele ya Angola.

Mirambo, juzi Jumatano alishuhudia Serengeti Boys ikichapwa na kupoteza mechi yake ya pili mbele
ya Uganda kwa mabao 3-0.

Awali, Serengeti Boys walipoteza mbele ya Nigeria kwa mabao 5-4. Mirambo ameliambia Championi Ijumaa kuwa: “Bado hatujakata tamaa, tutapambana mechi ya mwisho kuona tunatafanya vizuri kwa kushinda.

“Matokeo ambayo tunayapata kila mmoja yanamuumiza kwa sababu sisi hatukupanga iwe hivi, kitu kikubwa tunatakiwa tupambane kwenye mechi yetu hiyo ya mwisho na Angola.”

Share.

About Author

Leave A Reply