Sunday, August 25

Hakuna Heshima Kubwa kwa Mwanaume kama Mwanamke Kuutambua UUME wako Kabla hata Hamjakutana Kimwili.

0


Miaka 14 iliyopita nlikuwa kwenye Bus naelekea Arusha. Safari ilikuwa ya kikazi nmeondoka hapa Jumamosi kuelekea Arusha kuendeleza Ujenzi wa Taifa.

Binafsi huwa napenda kukaa siti ya nyuma ya dereva Dirishani. Siku hiyo bahati mbaya nlipata siti ya karibu na Korido. Lakini uzuri gari ilikuwa ni Two by Two ( Luxury Coach )

Nliwahi Ubungo kama kawaida nikawa nmeketi kitini na punde tu akaingia Dada mmoja mrembo sana na mwenye kunukia Utuli.akanisalimia Hi! Nikamjibu Hi! Nikampisha nikashusha kiti nimalizie Usingizi.

Hatukuweza kuongea tena sababu nlipokuja kuamka nlimkuta busy anasoma novel. Nami nikatoa novel yangu ya Danielle Steele sikumbuki jina. Huku nikiwa nmeweka Earphones masikioni nisisikie kelele za mle ndani kutokana na wao kuweka Movie ya Kinaijeria.

Liverpool. Hapa ndipo palipogeuza kila kitu katika safari hii iliyokuwa na ukimya kwangu.maana mara nyingi huwa namshawishi mkata tiketi aniwekee mtoto mzuri sitini kupunguza urefu wa safari.

Huyu nlikaa naye pamoja na uzuri wake na kuonesha ni mwanachuo kutokana na mazungumzo yake na maneno mama UE n.k halafu umareka mareka mwingi ( kuigiza uzungu) nliona hatutawezana maana alikuja ana nyodo zake tayari.

Baada ya yeye kula pale liverpool safari ilichukua kama saa moja hali kubadilika.huyu dada alianza kubadilisha mikao na kuna kipindi nlisikia kabisa hali ya hewa tumboni mwake haikuwa nzuri kutokana na ngurumo na baadaye akaanza kupiga radi ( alikuwa akijamba taratibu sana bila kelele)

Maskini mrembo yule katika harakati hizo za kupunguza gesi tumboni nadhani kuna vitu alitoa (wataalam wanashauri usitoe gesi tumboni ikiwa tumbo limechafuka na haupo maliwato)

Alishtuka.akaniita “kaka, kaka…” Nlitulia kwanza nipate uhakika kama ni mimi au siye aliponigusa nikatoa earphones na kumsikiliza.” Naomba unisaidie kile kibegi pale juu”

Nikawaza niinuke au niache.roho ya imani ikanijia “ada ya mja hunena uungwana ni vitendo” nikamletea.akatoa sijui kanga sijui kitenge au mtandio akajifunga.akamwita konda kuwa anaomba bus lisimame akajisaidie.

Dada mrembo alipatwa na safari ya mashaka mara ya nne anasimamisha gari abiria walianza kuja juu.nlisimama kiume na kuwauliza nani anafaham kuumwa na tumbo? Wakakosa la kujibu nikawa nawaza huu ndo muda wa kuchukua credit.basi mara nyingine nikawa nashuka naye huku sasa nampa maji yangu akanawie huko aendako.

Tulipofika sehemu flani imechangamka nlimwomba konda asimamishe bus nikanunue dawa kwa ajili ya mrembo. Alipokunywa dawa alishuka mara moja tu. Dawa ilionekana kumfaa.

Yule dada nlimhudumia kwa upendo na kumjali mpaka kufikia hatua akawa ananilalia kwenye mapaja.amepoteza nguvu kabisa.nambembeleza na nikampa juice yangu ya box ceres.akashukuru.

Alikuja kupokelewa na wazazi wake tulipofika moshi.hapo akanipa na namba yake ya simu mbele ya wazazi wake.ilibidi awaambie huyu kaka ndo kanisaidia.

Yule dada ndo alikuwa amemaliza chuo maskini.tukaendelea kuwasiliana na kuchat kwa mapenzi pasipo kutamkiana mapenzi.

Jana, kwenye moja ya vikao vya kikazi ndo kukutana na dada yule…aliponiona alinikimbilia akanikumbatia huku akisema ” yu are my man” watu walishangaa sana.

Miaka kadhaa ago alienda USA kusoma zaidi.tukapoteana. she came back 2017 hakujua anitafutie wapi maskini.email add nliyokuwa natumia nlisahau password nkafungua nyingine.tukapoteana.

Jana mbele za wenzie wawili alinipa credit ambayo ilinipa faraja sana ” mwenzenu sijawahi ona mwanaume kama huyu maisha yangu yooote, a perfect gentleman”

Nlitabasamu kimoyo moyo nikisema …hunijui wewe…subiri tu uone moto wake. Tumerudi kiurafiki upya kwa speed kubwa sana. Nkawaza je wenzangu mmewahi ku act gently kiasi mwanamke mwenyewe akashangaa kuwa bado kuna WANAUME WANAOJALI NA SI KUWA AMEZUNGUKWA NA MAFISI?

TUJIFUNZE. UANAUME NI MATENDO NA TREATMENT NZURI KWA WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE AU WASIOJIWEZA. SI KUPIGA GAME ZA KIBABE PEKEE. UANAUME SI MAUMBILE. NI MATENDO NA ROHO ILIYOKO NDANI

WABILLAH TAWFIQ
By GuDume


Share.

About Author

Leave A Reply