Sunday, August 25

Dr. Tulia Azitaka Shule Binafsi Kusaidia Watoto Wenye Uhitaji

0


Dr. Tulia Azitaka Shule Binafsi Kusaidia Watoto Wenye Uhitaji

Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanira Dr. Tulia Akson ameotoa wito kwa shule zote nchini hususani shule binafsi kujikita kusaidia watoto wenye uhitaji maalumu,kwa lengo la kuwawezesha kupata elimu jumuishi ili kuwafanya wajione sawa na watoto wengine na wenye umuhimu katika jamii.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Spika wa Bunge katika matembezi ya siku ya Usonji Duniani yaliyoandaliwa na Shule ya Al Muntazir jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wabunge ,yaliyobebaba kauli mbiu isemayo “TUWAPENDE NA TUWALIDE”.

Makumu MKuu wa Shule ya wasichana Almuntazir Mrs. Joan Soka akitoa utaratibu wa shughuli mbalimbali katika

Aidha Dr, Tulia amesema watoto wenye uhitaji maalumu wana haki sawa na wengine hivyo amezitaka shule binafsi kuweza kutoa mafunzo hayo kwa watoto wenye uhitaji maalumu kama inavyofanywa na Shule za Al Muntazir kwani itasaidia kuelimisha jamii kuhusu Usonji,(Autism) pamoja na kuwawezesha kuona kuwa watoto hawa wana haki ya kupata elimu na kuthaminiwa kama wengine.

” Jamii inapaswa kuwajali , kuwapenda na kuwalinda watoto wenye uhitaji maalumu wanauwezo wa kuelewa na kufanya vizuri darasani hata katika kazi mbalimbali kama kuchora kupaka rangi na wakifundishwa wanaweza hivyo jamii inapaswa kuwaona ni watoto wenye umuhimu kwa jamii hivyo wakiwezeshwa wanaweza kufanya zaidi”amesema

Watoto wenye usonji wakitoa burudani

Aidha Naibu Spika amewashauri viongozi wa Shule za Al Muntazir kujenga mabweni ya kuwawezesha watoto hao kupata sehemu ya malazi ili kuwawezesha watoto wenye uhitaji maalumu kutoka katika maeneo ya mbali kupata sehemu ya kulala,vilevile amezitaka Taasisi mbalimbali kujitokeza kutoa michango yao ili kuwawezesha watoto hao wasiokuwa na uwezo wa kuchangia gharama waweze kupata fursa ya elimu.

Spika wa bunge Dr Tulia akiteta jambo na rais wa shule za Al Muntazer.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr. Faustin Ndungulile ameishukuru shule hiyo kwa kuanzisha kitengo cha watoto maalumu na kuona umuhimu wa watoto hao kuwa wana haki ya kupata elimu kama wengine hivyo ameahidi Serikali itashirikiana kikamilifu endapo watahitajika.

Naye Mkurugenzi wa Shule za Al Muntazir Mahmood Ladak amewashukuru viongozi wa seikali pamoja na wazazi waliojitokeza katika matembezi hayo, na kusema lengo la matembezi hayo ilikuwa ni kuielimisha jamii kuhusu Usonji (AUTISM),na kuwapenda kuwathamini watoto wenye uhitaji maalumu,kwani wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.