Monday, March 25

Daimond Akabidhiwa Shule Sumbawanga

0


Daimond Akabidhiwa Shule Sumbawanga

Msanii Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka jiwe la msingi na kukabidhiwa Shule ya Senti ambayo wamemuomba iitwe jina la Diamond katika Mtaa wa Senti wilayani Sumbawanga leo, Jumamosi, Desemba 8, 2018.

Diamond amefanya tukio hilo alipokuwa ametembelea wilaya hiyo kwenye ziara yake ya muziki, ‘Wasafi Festival’ ambalo linategemewa kufanyika leo. Mradi wa shule hiyo umepungukiwa na kiasi cha Tsh. Million 68 ili kuweza kukamilika na shule ifunguliwe ifikapo Januari 2019.

Aidha, Diamond ameahidi kwamba kwa kiasi kilichobaki Watamalizia wote, “Mimi nathamini sana elimu na niwaahidi kitu kimoja kwamba, ujenzi huu uliyobaki, nitaumalizia wote,” aliahidi Diamond kwa wananchi mbele ya uongozi wa shule hiyo

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply