Tuesday, August 20

Binti Auawa na Tembo Waliokuwa Wakifukuzwa Shambani

0


Tukio hili limetokea usiku katika kijiji cha Bukore kata ya Kyambahi, ambapo binti wa miaka 26, Motondi Shakanyi ameuawa kwa kushambuliwa na Tembo

Kaka wa marehemu amesema kuwa alitoka yeye na mdogo wake wa kiume kwenda kuwafukuza Tembo hao kwa kuwapigia madebe

Anasema alimsihi Mama yake na mdogo wake huyo wa kike wabaki nyumbani na wasitoke nje lakini baada ya muda na wao walitoka na kuanza kuwafuata

Wakiwa njiani ndipo walikutana na Tembo aliyemnyanyua binti huyo na kumtupa umbali wa mita 5 na alifariki papo hapo 

Share.

About Author

Leave A Reply