Friday, July 19

Bifu la Fid Q, Babu Tale Ngoma Ngumu Babu Tale Amshauli Kununua Sabuni Aondoe Chunusi

0


Bifu la Fid Q, Babu Tale Ngoma Ngumu Babu Tale Amshauli Kununua Sabuni Aondoe Chunusi

RAPA maarufu Bongo, Faridi Kubanda Fid Q ameingia kwenye bifu zito na meneja wa msanii Diamond Platnumz, Babu Tale chanzo kikidaiwa kuwa ni tangazo la Tamasha Fiesta alilofanya msanii huyo na kudaiwa kwamba linakashifu Tamasha la Wasafi Festival.

Mameneja hao wametumia njia ya kumponda Fid Q kwa kuandika maneno ya kejeli kupitia mitandao ya kijamii; “Naskia gari hana na analelewa” ameandika Babu Tale katika ukurasa wake wa Instagram na ikanukuliwa kwamba Fid Q analelewa na mpenzi wake.

Rapa huyo hakukaa kimya, akajibu kupitia akaunti yake ya Instagram;

PART 1: @babutale Nimeonelea si vibaya nikifungua hiki kigazeti changu na sentensi hii. “ Keki ya taifa ni kubwa sana na ina vipande vingi vya kuwatosha wachakarikaji wote wenye kuistahiki, na kwakua Allah ndio mtoaji riziki, mimi kama mimi sina hayo mamlaka au hata hiyo roho mbaya ya kutamani wachakarikaji wenzangu mkwame katika harakati zenu.

Ninasema hivi ni kwasababu siku zote huwa siamini kama nitapungukiwa kitu nyinyi mkifanikiwa, na siamini hivyo kwa sababu ninajiamini mimi ni mchakarikaji na kipande changu cha KEKI bado kipo mezani kinaningojea ( cha muhimu ni PUMZI na DUA tu ).

Ni ukweli tupo kwenye tasnia moja na kila mmoja wetu anajaribu kufanya lile alionalo sahihi ili kusogea mbele, na iko wazi mmeshafanya na mnaendelea kufanya mengi makubwa, nami bila kusita siku zote nimekua ni mtu wa kuwapongeza iwe kwa njia ya mitandao au tukutanapo ana kwa ana.

Mie hufanya vile kiroho safi pasina chembe yoyote ya unafiki. Nimeyasema hayo hapo juu ili tu uweze au muweze kupata picha halisi ya kilichomo moyoni mwangu na pia kuwakumbusha ya kwamba mimi pia ninao uhuru wa kufanya shughuli zangu za sanaa na yeyote ambaye nimeridhia nae kimaslahi pasina kujali kama jicho la pembeni yangu linaiona faida iliyopo au laah.

Sioni ni busara kwa nyie kuja na kujaribu kunipangia yupi nifanye nae au yupi nisifanye nae ili kuwaridhisha machoni/ mioyoni mwenu. Na kama mnaamini ni haki yenu ya msingi mimi kuyafuata hayo matakwa yenu basi naomba nikujuzeni ndugu zangu mtakua mmeonyesha UBINAFSI wa hali ya juu kwenye hili. Pia kumbukeni mimi pia nishawahi kuwa na matatizo na MJENGO.

Lakini nilijikuta ninapambana peke yangu hadi UTULIVU uliporejea pasina msaada wa mtu yeyote. Na sikupambana peke yangu kwa sababu hamkua na taarifa, taarifa mlikua nazo lakini ninafikiri mlikua mmetingwa na shughuli zenu za ujenzi wa taifa kiasi kwamba hamkuona kama kuniongezea nguvu ingesaidia lile zoezi kuisha haraka.

Amini msiamini sijawahi kumuwekea mtu yeyote kinyongo kwenye hilo, na hiyo kitu ilinifunza sana juu ya suala zima la KUJIPAMBANIA MIE MWENYEWE kwenye situation yoyote ile na KUTOKUPIGANA VITA NISIYOIJUA au ISIYONIHUSU.”

PART 2: @babutale Yote na yote., kiukweli yale maneno ya kwenye promo ya “MOJA KUBWA” sikutegemea kama yangekua na uzito huu uliopelekea ndugu yangu uchafukwe kiasi cha kunifungulia bomba la matusi humu insta.

Kwanza sikumbuki hata kama niliyatamka kwa nia ya kuleta msigishano huu. Lakini kama kweli nimewakwaza. Naomba mnisamehe kibinadamu kwa hilo, naomba tumuache SHETANI apite na mwisho naomba nimalize kwa kusema. BURUDANI sio VITA, hivyo ninawatakia kila la heri/ MAFANIKIO ya hali ya juu katika MAPINDUZI YA BURUDANI huko MTWARA.. KEKI”.

TAZAMA HAPA CHINI VIDEO MPYA YA ROSA REE-BANJUKA


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply